BARKER KOCHA MKUU SIMBA SC

SIMBA SC imemtangaza Kocha kutoka Afrika Kusini STEVEN VAN BARKER kuwa Kocha wake Mkuu akichukua nafasi ya DIMITAR PANTEV ambaye alifurushwa hivi karibuni. Barker aliwahi kuwa Kocha wa Stellenbosch ya Afrika Kusini na walicheza na Simba Nusu fainali ya CAFCC msimu uliopita.

Barker amewashinda Erick Tinkler na Amine El Lkarma ambao aliingia nao 3 Bora. Mchakato wa Simba ulivutia makocha wengi wa ndani na nje ya nchi akiwemo Romain Folz na Miguel Garmond ambao wote waliwahi kufundisha Yanga SC. Garmond kwa sasa ni Kocha wa Singida Big Stars na Kocha wa muda wa Taifa Stars.

Scroll to Top